Njia za kuepuka harufu mbaya ya kwapa

Njia za kuepuka harufu mbaya ya kwapa

 

Ulimwengu wa fashion umebebwa na vitu vingi sana huku umaridadi na usafi vikiwa ndiyo nguzo yake. Katika jamii zetu ni suala la aibu kukuta mtu kapendeza lakini akawa anatoa harufu mbaya ya kwapa. Mara nyingi hata upendeze vipi kitu kimoja tu kinaweza kukupotezea sifa zote.

Kwa kulitambua hilo Mwananchi Scoop tumekusogezea makala inayohusu njia mbalimbali za kuepuka harufu mbaya ya kwapa. 

Usafi wa mara kwa mara, unashauriwa kuosha kwapa kwa sabuni yenye antibacterial mara mbili kwa siku ili kuondoa jasho na bakteria. Ni muhimu kuhakikisha kwamba eneo hili linakuwa kavu baada ya kuoshwa.

Matumizi ya Deodorant au Antiperspirant, deodorant inaweza kusaidia kuficha harufu mbaya, wakati antiperspirant huzuia uzalishaji wa jasho. Chagua bidhaa ambazo zinaongeza ulinzi dhidi ya harufu na jasho. 

Mavazi ya pamba, ukiwa na tatizo hilo unashauriwa kuvaa nguo zinazotengenezwa kwa nyuzinyuzi za pamba, kwani zinapumua vizuri na husaidia kuondoa unyevu, ikilinganishwa na nyuzinyuzi nyingine kama vile polyester.

Matumizi ya poda, zipo maalum kwa matumizi ya mwili inaweza kusaidia kufuta unyevu na kupunguza harufu. Hakikisha unachagua poda isiyo na madhara kwa ngozi yako.

Kula chakula bora, chakula unachokula kinaweza kuwa na athari kwa harufu ya mwili wako. Epuka chakula kilicho na viungo vingi kama vitunguu na pilipili, kwani vinaweza kuchangia harufu mbaya ya mwili.

Kunywa maji ya kutosha, maji mengi husaidia kutoa sumu mwilini kupitia mkojo na kuzuia harufu mbaya inayotokana na jasho.

Licha ya hayo yote ni muhimu kumuona mtaalamu. Ikiwa tatizo linaendelea licha ya kufuata hatua hizi, inaweza kuwa na uhusiano na hali ya kikinga au hali ya kiafya. Katika hali hiyo, ni muhimu kumuona daktari au mtaalamu wa ngozi kwa ushauri zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags