Njia bora za kushinda au Kukabiliana na hofu

Njia bora za kushinda au Kukabiliana na hofu

Watu wengi wanakabiliwa na kuathiriwa na hofu katika maisha yao kwa namna moja au nyingine. Hofu hizi zinaweza kusababishwa na mazingira, mtu, kitu au hata sababu za kisaikolojia.
Hofu isiposhughulikiwa kwenye maisha inaweza kuwa kikwazo kikubwa cha mafaniko ya mtu husika, wengi wanatamani kukabiliana na hofu lakini bado hawajui namna ya kuweza kukabiliana na jambo hilo.
Je uko tayari kushinda hofu sasa, karibu nikushirikishe njia bora ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na hofu maishani mwako.
Punguza au ondoa mawazo na imani potofu
Wakati mwingine watu wanapata hofu kutokana na imani au fikra potofu pekee. Kwa mfano unaogopa kinyonga kwa sababu umesikia kuwa kikukugusa utatokwa na ngozi au kufa, ju una uhakika juu ya swali hili?
Maswala mengi yanayowaogopesha watu ni kutokana na imani potofu tu na wala hakuna ukweli wowote, chunguza kama kweli swala linalokupa hofu ni la kweli au ni fikra na imani potofu tu.


Kizoee kile kinachokupa hofu
Kukikimbia kile kinachokuogopesha hakuwi suluhisho la hofu yako bali huifanya iimarike zaidi. Kwa mfano ikiwa unaogopa mbwa, basi ukimwona mbwa usikimbie kaa na jitahidi kumzoea.
Kwa njia hii baada ya muda utaweza kukizoea kile kinachokutisha na hutokuwa na hofu tena unapokutana nacho.


Tafakari madhara ya hofu
Hebu fikiri jinsi hofu itakavyoathiri ufanisi na utendaji wa kazi zao, usikubali hofu ionekane kubwa kuliko madhara yake.
Kama hofu huzuia kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi ule unaotakiwa kwanini itutawale? Kwa mfano ikiwa una hofu ya mtihani, umeshawahi kufikiri jinsi hofu hiyo itakavyokuathiri katika mitihani yako kuliko hata kilichokuwa kinakutisha kwenye mtihani wenyewe.
Fikiri tofauti sana, usikubali hofu ikutawale kuliko athari zake. Ukizingatia hili hutoogopa tena hofu bali utaiepuka kwani hutokubali iathiri kile unachokifanya.


Usijaribu kuwa mkamilifu
Kila mtu ana mapungufu yake, hivyo kuogopa kwa ajili ya udhaifu fulani au kujitahidi kuepuka hofu ili uwe mkamilifu ni makossa.
Tambua udhaifu wako na ukubali ili uweze kukabiliana nao. Epuka kuhofu mambo ambayo hayana sababu. Tambua kila mtu ana udhaifu wake, tofauti yetu ni namna tunavyokabiliana na udhaifu huo pekee.


Kumbuka mambo au maeneo ya furaha
Njia nyingine ya kukabiliana na hofu ni kujikumbusha mambo au maeneo ya furaha. Mara unapopatwa na hofu jikumbushe eneo au jambo ambalo huwa linakupa furaha na ujasiri.


Kumbuka tunavyofikiri ndivyo tunavyokuwa, hebu jitahidi kutafakari jinsi lile eneo au jambo lingine linavyokupa furaha na amani kuliko hata hilo dogo linalokupa hofu.
Fikiri pia jinsi ulivyokutana na mambo mengine yaliyokupa hofu kwenye maisha yako lakini yakapita bila tatizo lolote hivyo usikubali hofu yoyote kutawala fikra zako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags