Njia bora ya Unyoaji Ndevu kuepuka Vipele

Njia bora ya Unyoaji Ndevu kuepuka Vipele

Karibu tujuzane mambo mbalimbali kuhusiana na masuala ya urembo, mitindo na mavazi ambayo najua uwenda unayajua ila mimi nakujua zaidi.

Msomaji wetu leo tutaangalia juu la hili suala la unyoaji wa ndevu kwa wanaume.

Moja ya matatizo makubwa kwa wanaume ni madhara wanayoyapata wakati wa unyoaji wa ndevu hasa utokwaji wa vipere, kwani jambo hilo wakati mwingine huwakera wahusika.

Ili kuondoa matatizo unayoyapata wakati wa unyoaji huo, fanya haya yafuatayo yanaweza kukusaidia kukuweka katika aina fulani ya raha.

Kwanza, unapaswa kuchagua mashine ya kunyolea na wembe ambao unadhani unaswihi ngozi yako, najua zipo aina nyingi sana za mshine pamoja na nyembe zake lakini ni muhimu kujua wembe ambao unatumia utazingatia mahitaji yako hasa ya aina ya ndevu ulizonazo.

Pili, weka uso safi kwa kuusafisha kabla ya kunyoa hii itakusaidia kufungua matundu yanayoshikilia ndevu kabla ya kunyoa ili kuweza kupata mnyoo laini na wenye uhakika.

Tatu, usisahau kuloweka kidevu chako vyema hii itasaidia wembe kupita kiulaini zaidi na kama unatumia kiwembe cha kawaida basi ni vyema sana kufanya kazi hiyo ukitoka kuoga.

Nne, Tumia maji ya moto siyo yanayounguza kama itawezekana kwani yanasaidia sana kufungua vishimo vya vinyweleo pia unaweza kupata masaji ya haraka katika uso ambayo usaidia kulainisha kidevu chako.

Tano, chagua krimu ya kunyolea inayostahili kwako ambayo itatengeneza ngozi yako jipake kiasi cha kutosha katika sehemu zinazostahili kwani husaidia kuburudisha ngozi. Baada ya kunyoa osha uso wako kwa maji safi na ondoa krimu zote.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags