Nigeria kufunga mipaka siku ya uchaguzi

Nigeria kufunga mipaka siku ya uchaguzi

Uchaguzi wa rais na bunge nchini Nigeria unaripotiwa kuwa na upinzani mkali zaidi tangu utawala wa kijeshi kumalizika mwaka 1999, hivyo basi nchi hiyo imeamuru kufungwa kwa mipaka yake yote ya ardhi wakati wa uchaguzi utakaofanyika kesho Jumamosi wenye ushindani mkali.

Idara ya Uhamiaji ya Nigeria ilisema kuwa Maagizo hayo yanalenga kuhakikisha kuwa uchaguzi huo ni huru, wa haki na hauna dosari, Maafisa wa mpaka wameambiwa kuhakikisha utekelezwaji mkali wa agizo hilo.

Idara ya uhamiaji ilisema imekamata kadi za wapiga kura 6,000 na hati nyingine za utambulisho wa Nigeria kutoka kwa wahamiaji haramu katika kipindi cha maandalizi ya uchaguzi.

Aidha Rais Muhammadu Buhari mapema Alhamisi alivitaka vyombo vya usalama kuwa imara na ujasiri katika kipindi cha uchaguzi, na kuonya dhidi ya ghasia baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags