Nicklass: Kuwa director mzuri kunahitaji push ya wasanii

Nicklass: Kuwa director mzuri kunahitaji push ya wasanii

Guys!! This is onather weekend mtu wangu wanguvu I hope uko poa na ulikuwa una subiria segement yetu ya burudani na michezo, sisi hatuna baya lazima tukuelekeze nini kimehappen wewe usicho kijua mwanetu.

Leo bhana katika burudani tumekuletea safari ya Director Nicklass, maisha yake akiwa kama director si unajua tena kila mtu ana background yake na historia lazima tukujuze mwenetu.

Kwanza kabisa kabla sijakupa utamu tunafahamu kabisa hapa Tanzania kuna madirector kama wote na kila mtu ana talanta na ujuzi katika kutengeneza video mbalimbali lakini leo Mwananchi Scoop ikamsanukia Director wa video mbalimbali za muziki, Nicklass Mbaga.

Nicklass amezaliwa mkoa wa Dodoma mvumi ila kutokana mzee wake alikuwa mwalimu na mtumishi wa serikali hivyo walihama kijiji cha mvumi na kwenda Dodoma mjini hapo ndipo alipo anzia elimu yake ya awali na kumalizia elimu yake ya juu mkoa wa Iringa.

Anaeleza alipo kuwa chuo ndio safari yake ya kutengeneza video ilipo anzia, alianza kwa kuedit picha za wanafunzi wenzie huku akiwatengenezea beat mbalimbali katika matamasha yaliokuwa yanatokea chuo anasema.

“Kuna mtu alinipa app ya kuediti picha na hapo nilikomaa kujua nakumbuka nilianza kuediti picha yangu mimi mwenye nikatengeneza picha niko mimi, Snoop Dog na Mwana FA hahahaha!!” alisema Niko.

Anaendelea kueleza “Kwa miaka ile wana walikuwa wanashangaa sana ebana hii inakuaje hapo sasa ndipo nilipoanza kupenda Art kurudi kwenye kupiga mabeat nikaona si sifiwi ikabidi niegemee upande ninao sifiwa, kuendelea kutengeneza picha na Logo nanilikuwa na pata pesa”

Alifanya video yake ya kwanza mwaka 2010 ilikuwa ya washkaji zake huku hakuwa anategemea kama kitakuwa ni kitu kikubwa watu watakapo iona kipindi hicho alikuwa akitumia digital Camera ndogo anasema.

“Video ilipokuja kutoka hakuna alie amini kama nilikuwa nimefanya mimi ilikuwa kali halafu kwa upande wangu sikupata shida kuitengeneza nilikuwa nikichukulia rahisi tu”

Baada ya kupewa sifa na watu walio kuwa wakiona kazi zake hapo alianza kupenda zaidi kutengeneza video ila baadae alizama kwenye upande wa photography akideal na picha za fashion na wedding.

Pesa yake ya kwanza kuishika aliweza kununulia camera yenye wezo mkubwa kwa miaka hiyo kwajili ya kazi zake anaeleza.

“Kuna mwanangu mmoja alikuwa ajui kuimba lakini alikuwa anapenda nikamshauri nimtengeneze video ya nyimbo yake mimi nikiwa najaribu je video itaenda kama ile ya mara ya kwanza, video ilivyotoka ilikuwa nzuri sana nikazidi kuweka userious” alisema mwamba huyo.

Hakuwa anaamini kwamba ipo siku atafanya vitu kikubwa na atakubalika na wasanii kwasababu alikuwa akiona ni aina ya watu ambao walikuwa wameandikiwa kuwa hivyo na sio yeye.

“Nakumbuka kuna siku Jonh Mkini alikuja Iringa ilikuwa mwaka 2013 kuna video aliiona nilikuwa nimefanya hakuamini kama imefanyika mkoani” alisema Nicklass.

Japo kuna baadhi ya watu walikuwa wakimtabiria kuwa atakuja kuwa director mkubwa akiwemo Amosi Mwijonge mtunzi wa mashahiri.

Licha ya hayo anaeleza shabiki yake mkubwa ni mama yake mzazi na alikuwa akimsaport kila hatua anayopiga katika talanta yake anasema Director huyo.

“Kuna kipindi mama alivyoona nazidi kufanya vizuri akaninunulia Camera kubwa ambayo sijui pesa alitolea wapi maana ilikuwa ya gharama mpaka leo hii mtu wangu wa kwanza kuangalia kazi zangu kabla hazijatoka ni mama angu”

Kama tunavyojua katika utafutaji lazima kuwe na changamoto amabazo zitakazo kufanya uimarike zaidi katika kutafuta kwako mafanikio lakini Niko anaeleza.

“Nilipata ugumu nilipoanza kuja kufanya kazi Dar mambo yalikuwa magumu nilikuwa nawajibika kuwa muonekano mkubwa kushinda uwezo wangu ilinipate kazi za wasanii wa kubwa kipindi hicho kama Mr Blue alikuwa anapenda kutazama muonekano wa director”

Anaendelea kueleza “So ilikuwa inanilazimu kutumia gharama kubwa kuwa katika mtindo wa kisuper star kuna kipindi nilikuwa na lala njaa lakini mwisho wa siku nikajitafuta mpaka nikajipata”

Kingine usicho kijua kwa huyu mwamba napenda sana kukaa peke yake akitafakari kitu kipya ambacho akikipeleka katika timu yake ambayo wanafanyakazi kwa kushirikiana wana kikubali anasema.

“Kuna time msanii anakuja kutaka ushauri kwenye video yake sasa hapo kama hamna kitu kipya unakuwa unapotea, wasani wanataka Director awenauwezo mkubwa kiasi kwamba akikwama kimawazo aweze kupata msaada kutoka kwa Director” alisema Nicklass.

Mwisho kabisa alimalizia kwa kusema ndoto yake kubwa nikutambulika na kuwa director mkubwa wakimataifa anaeleaza.

“Mimi nataka kuwa mkubwa nitambulike kimataifa lakini ili nifike huko push ya wasanii kufanya mziki mkubwa zaidi na mimi director ndio nitaonekana”

Siku zote huwaga nawaambia kila mtu na kitu chake binafsi ambacho akifanya kitawashangaza wengine hasa kwenye talanta, mwanetu wewe ni special amua kwanzia leo kuthubutu, kama kawida till next weekend.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags