Nicki Minaji aachia kionjo cha kolabo na Burna Boy

Nicki Minaji aachia kionjo cha kolabo na Burna Boy

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Nicki Minaj kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share kionjo cha ngoma yake ambayo ameifanya na mkali wa #Afrobeat kutoka Nigeria, Burna Boy.

Imeelezwa kuwa wawili hao watafanya remix ya ngoma ya Burna Boy ya ‘Tested Approved & Trusted’ ambayo ina miezi mitano tuu tangu kuachiwa kwake, ikiwa na wasikilizaji zaidi ya milioni 17 kupitia mtandao wa #YouTube.

Hii siyo mara ya kwanza kwa #BurnaBoy kufanya ‘kolabo’ na ma-staa wa Kimarekani awali aliwahi kufanya ngoma na ‘rapa’ #J.Cole katika wimbo wa ‘Thank’, na ile ya #21Savage ‘Just like me’.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags