Nicki Minaj asimamisha show kumpongeza Davido na Chioma

Nicki Minaj asimamisha show kumpongeza Davido na Chioma

‘Rapa’ wa Marekani Nicki Minaj wakati akiwa anatumbuiza kwenye tamasha la ‘Afro Nation 2024’ lililofanyika nchini Ureno alisimamisha show yake na kumpongeza mkali wa Afrobeat Nigeria Davido na mke wake Chioma.

Wakati alipokuwa kwenye show hiyo mwanamuziki huyo aliwapongeza Davido na Chioma kwa hatua kuwa ya kufunga ndoa huku akitumbuiza ngoma ya ‘Holy Ground’ alioshirikishwa na Davido ya mwaka 2020.

Aidha kufuatia na ngoma hiyo kupigwa kwenye show hiyo inadaiwa kuwa imerudi kwenye chati za iTunes nchini Ureno kwa kushika namba moja, vile vile inatajwa kurudi tena katika chati kwenye nchi tofauti zikiwemo Nigeria, Swaziland, Ghana na kwingineko.

Utakumbuka kuwa Davido na Chioma walifunga ndoa siku ya Jumanne Juni 25, 2024 nchini Nigeria huku ndoa yao iki-trend ndani na nje ya Afrika.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags