Nicki Minaj ampisha Lil Wayne kwenye soko la muziki

Nicki Minaj ampisha Lil Wayne kwenye soko la muziki

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, #NickiMinaj amesogeza mbele tarehe ya kutoa albumu yake ya ‘Pink Friday 2’ kutoka Novemba 17 hadi Disemba 8 mwaka huu ambayo itakuwa ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake.

Inaelezwa kuwa ‘rapa’ huyo ametaja moja ya sababu ya kusogeza mbele tarehe ya kutoa albumu hiyo ni kwa ajili ya kupisha albumu ya #LilWayne iitwayo ‘Welcome 2 ColleGrove’ ambayo imetangazwa kutolewa Novemba 17.

Wasanii hao wa hip-hop Nicki na Lil Wayne waliwahi kufanya ‘kolabo’ mbalimbali ikiwemo wimbo wa ‘High School’ walioufanya miaka kumi iliyopita.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags