Ngono zembe yaongeza kasi maambukizi ya VVU kwa vijana

Ngono zembe yaongeza kasi maambukizi ya VVU kwa vijana

Chuo kikuu cha Aga Khan jijini #Nairobi nchini Kenya kimebaini kufanya ngono zembe kwa vijana kumeongeza kasi ya maambukizi ya nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika chuo hicho cha Afya inaelezwa kuwa chanzo cha watoto waliozaliwa na maambukizi ya VVU, ambayo sasa ni vijana au watu wazima wamekuwa wakijihusisha na ngono bila kuchukua tahadhari.

Aidha Dkt. Adeel Shah, Bingwa wa magonjwa ya kuambukiza na watoto kutoka #AgaKhan amesema "vijana hawa wamekuwa kundi la maambukizi, wanaingia kwenye mahusiano na wenzao wasio na VVU na kushiriki ngono bila kinga, hali inayowaweka watu wengi zaidi katika maambukizi"

Hata hivyo sababu nyingine ni vijana waliogeuza miili yao kama kitega uchumi kwa kujihusisha na ngono na watu wazima kwa lengo la kujipatia fedha, matokeo yake wengi wameishia kupata maambukizi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa kwa sababu wanaokutana nao wanawapa masharti ya kutotumia kinga.

Ripoti mpya ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI nchini humo, imeonesha ongezeko la watu takribani 32,017 huku vijana wakiwa 11,229 na wengi wao ni wenye umri wa miaka kati ya 15 hadi 24.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags