Neno Hakuna Matata aendelea kutikisa kwenye sanaa

Neno Hakuna Matata aendelea kutikisa kwenye sanaa

Neno la Kiswahili Hakuna Matata, linaendelea kutikisa kwenye nyimbo za wasanii kutoka Marekani baada ya mwanamuziki Gunna kutoka nchini humo kuachia wimbo unaoitwa Hakuna Matata, siku tano zilizopita.

Hii inakuwa ni mara ya pili neno hilo kutumika kama jina la ngoma za wasanii kutoka Marekani, ambapo kwa mara ya kwanza lilisikika mwaka 2018 kwenye ngoma iliyoimbwa na wasanii Ernie Sabella na Nathan Lane.

Inafahamika kuwa "Hakuna Matata" limetokana na lugha ya Kiswahili, likiwa na maana ya kuwa "hakuna shida" au "hakuna wasiwasi".
Neno hili liliongeza umaarufu baada ya kutumia kwenye filamu ya Disney ya mwaka 1994 "The Lion King".

Katika filamu hiyo, wahusika wawili, Timon na Pumbaa, wanatumia neno "Hakuna Matata" kuelezea fikra yao ya kuishi bila wasiwasi.

Kutokana na kupata umaarufu huo ikapelekea neno hilo kuwa miongoni mwa maneno ya Kiswahili yanayofahamika zaidi duniani. Mbali na kutumiwa na wasanii hao wa nje msanii wa Tanzania Marioo naye hivi karibuni ameachia ngoma yenye jina hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags