Ne-Yo aiomba mahakama Ex wake kutozungumzia kesi yao

Ne-Yo aiomba mahakama Ex wake kutozungumzia kesi yao

Baada ya kutangazwa kuwa baba halali wa watoto wawili ambao ni Braiden na Brixton, msanii Ne-Yo ameripotiwa kuiomba mahakama isimruhusu ex wake Sade Bagnerise kuzungumza hadharani kuhusu ‘kesi’ yao.

Kwa mujibu wa Radar Online, Ne-Yo alidaiwa kuiambia Mahakama kuwa yeye ni msanii wa kimataifa mwenye rekodi za heshima hivyo basi anahitaji mjadala huo kufungwa na kuiomba mahakama impige marufuku ex wake kujadili mwenendo wa kesi yao katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Aidha Sade alikubaliana na ombi hilo la kutokuzungumza chochote katika vyombo vya habari na kupelekea wawili hao kufanya makubaliano ya malezi ya watoto ambapo Ne-Yo ataruhusiwa kuwaona watoto kila weekend pia atatakiwa kulipa pesa ya matumizi ya watoto.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags