Ndoto ya Lebron James kucheza na mwanaye yatimia

Ndoto ya Lebron James kucheza na mwanaye yatimia

Gwiji wa mpira wa Kikapu wa Marekani, LeBron James anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kucheza ‘timu’ moja na mwanawe wa kwanza, Bronny James.

Mpango huo umewezekana baada ya ‘timu’ ya Los Angeles Lakers kumsajili Bronny mwenye umri wa miaka 19, akitokea katika ngazi ya michuano ya vyuo nchinu humo.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa, ilikuwa kiu kubwa kwa LeBron James kucheza timu moja na mwanawe, baada ya kusubiri hilo kwa miaka 21 iliyopita.

Uteuzi huo unafungua njia kwa baba na mwana kucheza kwa wakati mmoja katika NBA huku Bronny, akijiandaa kwa msimu wake wa kwanza na LeBron, akijiandaa kwa mara yake ya 22.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags