Ndoa yaingia doa, Bibi harusi adakwa na polisi

Ndoa yaingia doa, Bibi harusi adakwa na polisi

Bibi harusi kutoka nchini Mexico aitwaye Nancy N amekamatwa na polisi siku ya harusi yake kwa tuhuma za unyang’anyi.

Nancy N alikamatwa wakati alipokuwa akishuka kwenye gari akiwa anaelekea kanisani huku mumewe mtarajiwa aitwaye Clement N, akifanikiwa kutoroka.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa wawili hao na wengine sita wanatuhumiwa kwa kufanya unyang’anyi kwa wafanyabiashara wa kuku mji mkuu wa Mexico.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwateka wafanyabiashara wa maduka ya kuku na kuchukua kuku kisha kuwafungia katika ghala. Ofisi ya mwendesha mashtaka imeweka wazi kuwa uchunguzi bado unaendelea.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags