Ndoa ya Nandy na Billnass yavutia mashabiki

Ndoa ya Nandy na Billnass yavutia mashabiki

Kwa #Bongo ukizungumzia penzi la watu maarufu ambalo limedumu hadi kuingia kwenye ndoa huwezi acha kumzingumzia #Nandy na #Billnass.

Wanandoa hao unaweza kuwaita ndege wawili wapendanao warukao pamoja, wamefanikiwa kufikisha mwaka mmoja katika ndoa yao, licha ya vikwazo na changamoto ambazo ziliwahi kutokea huko nyuma, ambazo baadhi ya watu wamekuwa wakizitumia kama silaha ya kuwapigia.

Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata ndoa ya watu maarufu ambayo inafananishwa na ndoa ya #Beyonce na #Jay-Z.
Hivi juzi kati kwenye harusi ya #Barnaba mashabiki wengi walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakifananisha ndoa ya #Nandy na #Nenga na ndoa maarufu duniani ya #Beyonce na #Jay-Z kutokana na kuendana na kupendana kwao.

Huku wengine wakitupa jicho kwenye kichwa cha #Nenga na kujadili nywele ya mkali huyo ambayo ilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, huku kila mtu akifananisha nywele hiyo na kile anacho kifahamu.

Ndoa ya mastaa gani wengine #Bongo inakuvutia?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags