Nay: Muziki wangu haulengi watu wa mtandaoni

Nay: Muziki wangu haulengi watu wa mtandaoni

Akizungumza na shirika la habari BBC mwanamuziki wa Hip-hop nchini Nay wa Mitego amedai kuwa muziki wake huwa anawalenga watu wenye hali ya chini kabisa hivyo anachanganyikiwa pale wimbo wake usiposikika mtaani ambako yeye anaamini kuna watu wenye kipato cha chini.

 Nay hachanganyikiwi muziki wake ‘usipohiti’ mtandaoni kwa sababu muziki wake haulengi watu wa mtandaoni ila akili yake inamruka pale muziki usipo wafikia mashabiki wake mtaani wenye hali za duni.

 Akidai kuwa mashabiki wake wa mtaani wenye hali ya chini wanaweza kuingia mtandaoni mara moja kwa wiki, sasa ili muziki wake umfikie shabiki yake lazima yeye mwenyewe au-push uwafike mtaani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags