Nenga amesema kwamba Nay alitaka afungwe jela hivyo ameendelea kujifungia ikiwa ni pamoja na kumzuia mke wake Nandy kushirikiana na Nay.
"Hamna hata shida kubwa kwa sababu wakati inatokea alitamani mimi niende jela, kwahiyo mimi bado nipo jela nimejifungia kule ambapo alitaka niwepo, sijafanikiwa kwenda jela alipotaka lakini bado nipo alipotaka kimaono" amesema Billnass
Hata hivyo, Nay amemjibu Nenga kupitia upande wa comment wa chapisho hilo akisema Nenga ni mwizi na angeenda jela kwa tabia yake hiyo.

"Msanii mjinga ambae amekua anapenda trending kwa style yoyote ile aya acha nikupe unachotaka wewe ni mwizi ungeenda jela kwa tabia yako ya wizi. Nina kazi nyingi za kufanya nianze kukukandamiza wewe kwenda jela how yani.?! Mgande Nandy ivyo ivyo ili usije ukaendelea na udokozi.!!" ameandika Nay
Leave a Reply