Namna ya kupika visheti vya sukari kwa ajili ya biashara

Namna ya kupika visheti vya sukari kwa ajili ya biashara

Na Aisha Lungato

Novemba kama Novemba, niliwaambia siku hazigandi bwana, na tumebakiza mwezi mmoja tuu tumalize mwaka, haya ndugu yangu vacation unaenda na pesa gani bila ya kuchakalika.

Kama wanavyosema kazi na dawa basi biashara nayo ni kazi, so fanya ufanyavyo lazima mwisho wa mwaka ukamwagilie moyo, haya tuachane na hayo turudi kwenye biashara sasa leo nimewashushia pishi ambalo linapendwa sana na wanafunzi.

Visheti ni aina ya kitafunwa ambacho unaweza kunywea na kahawa, chai na hata juice na bei yake ni kuanzia 200 mpaka 500, so ukipata sehemu ya shule utakuwa umeua sana.

Haya ungana nami mwanzo mpaka mwisho kujua dondoo la pishi hili.

Mahitaji

  • Unga wa ngano 1⁄2kg
  • Nazi iliyokunwa isage kwa blenda kupata tui laini (kifuu 1)
  • Pinch ya chumvi
  • Beaking powder 1tsp
  • Hamira 2tsp
  • Mafuta kijiko kimoja
  • Hiliki iliyosagwa kijiko kimoja kidogo

Jinsi ya kuandaa

  • Changanya unga beaking powder hamira na chumvi na hiliki kisha weka nazi yako iliyosagwa na mafuta kanda unga wako tumia tui la nazi kukandia hakikisha unakuwa laini kama wa maandazi ukande vizuri kisha uache uumuke.
  • Ukisha umuka tengeneza shape ndogo ndogo (Kama hivyo pichani)
  • Panga kwenye working table yako ziumuke kisha weka mafuta jikoni yakipata moto pika kama maandazi, kwa moto wa chini ili ziive vizuri.

Namna ya kuandaa shira

Najua mnajua kuandaa shira lakini wacha tuendelee kupeana ujuzi.

➢ Chukua sufuria kubwa, tia maji robo kikombe, sikari kikombe kimoja, hiliki kisha weka jikoni ichemke mpaka ianze kunata.

➢ Tia visheti vyako uvipete mpaka sukari igande kama vinavyoonekana kwenye picha hapo. Na mpaka kufikia hapo vitakuwa tayari kwa kuliwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post