Namna  ya kupika burger ya nyama ya ng’ombe

Namna ya kupika burger ya nyama ya ng’ombe

Aiseee!! Wacha kabisaa wewe ukisikia mambo mazuri mambo matamu ndiyo hayo sasa this week kwenye Nipe dili nimekuletea jinsi ya kupika baga ya nyama ya ng’ombe unajua kuandaa?

Hatari sana karibu nikufahamishe process zote yaani ushindwe wewe tu kuonyesha ufundi wako bwana au vipi? Twende sote tukianzia na mahitaji yake. 

Mahitaji

Nyama ya kusaga (mince beef 1/4 kilo)
Yai (egg 1)
Unga wa mkate (bread crumbs 2 vijiko vya chai)
Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic paste 1/2 kijiko cha chai)
Kitunguu maji (onion 1)
Tangawizi iliyosagwa (ginger paste 1/2 kijiko cha chai)
Nyanya (fresh tomato 1)
Tango (cucumber 1/4)
Lettuce
Chumvi (Salt 1/2 kijiko cha chai)
Ketchup
Mayonnaise
Burger bun (mikate ya burger 3)

Matayarisho


Weka nyama kwenye bakuli kisha tia chumvi, yai, unga wa mkate kitunguu swaum,tangawizi na pia kitunguu maji (kikate vipande (cubes ndogo ndogo) na kisha uichanganye vizuri na uitawanyishe katika madonge 3.

Baada ya hapo iache imarinate kwa muda wa dakika 30 na itakuwa tayari kwa kupikwa. Unaweza kuipika katika jiko la mkaa kwa kuweka wavu wa kuchomea nyama katika moto wa wastani, Pika upande mmoja mpaka uive na kisha ugeuze upande wa pili na pia uupike mpaka uive


Ikiwa hauna jiko la mkaa unaweza kutia kwenye oven na uigrill kwa muda wa dakika 15 kila upande katika moto wa wastani mpaka hapo baga itakapoiva.


Baada ya hapo andaa mkate wa burger kwa kuukata kati kisha katakata (slice) tango, kitunguu,nyanya na lettice.Kisha anza kuvipanga kwenye mkate wa burger kwa kuweka lettice chini kisha tango,nyanya, vitunguu na kisha burger yenyewe. Baada ya hapo tia mayonnaise na ketchup juu ya burger na upange tena vitunguu, nyanya, tango na lettice.

Kisha  weka mkate wa burger kwa juu na burger itakuwa tayari kwa kuliwa

Unaweza pia kuandaa na chips pembeni ili kunogesha baga yako wakati wa kulaaa!!.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags