Namna ya kupika biscuit aina ya cookies

Namna ya kupika biscuit aina ya cookies

Hellow!  i hope mko poa watu wangu wa nguvu, kama kawaida yetu katika segment ya biashara tunakushushia vingi hatari ili na wewe usikae kinyinge.

Katika biashara leo nimekusogezea namna ya kutengeneza Cookies, kwa wale wasiozifahamu ni aina ya biscuit ambazo unaweza kunywa na juice au kahawa, na hizi mara nyingi huuzwa katia package yake maalumu na bei yake pia imechangamka haswaaa.

Haya ungana nami mwanzo mpaka mwisho kujua namna ya kutengeneza biscuit hizo ambazo hupendelewa na watu tofauti tofauti.

Mahitaji

-        Butter au blue band robo

-        Sukari laini robo

-        Unga wa ngano robo

-        Baking poder kijiko 1

Jinsi ya kuzitengeneza kwa kuoka

-        Chukua Bluband yako au butter na sukari vichanganye mpaka viwe laini kabisa

-        Chukua unga wako changanya na baking poder kisha changanya na mchanganyiko wako wa bluband na sukari usitie maji kabisa maana hizi zinatengenezwa na mahitaji hayo matatu tuu.

-        Kisha uache kwa dakika 20, kisha kanda kidogo na uanze kukata shape uzipendazo.

-        Ukimaliza hapo washa oven ipate moto kwanza na utaoka kwa dakika 15 hadi 20 na mpaka kufikia hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa na kuuzwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags