Namna ya kupanga malengo ukiwa kazini

Namna ya kupanga malengo ukiwa kazini

Hellow! I hope mko good watu wangu wa nguvu, haya sasa tunaamia upande wa pili naona katika suala la interview (usaili) tumemaliza sasa nawaomba wote tuhamie huku.

Yaani nataka kuwapa vitu mpaka mkifika kazini waajiri wenu waulize yote haya mmeyapata wapi, nataka ukifika kwa boss akikuona aone kuwa amepata mfanyakazi ambaye ataendana naye kwa kila hali.

Malengo ni kitendo ambacho kila mwanadamu lazima awe nacho sasa kama wewe mwenzetu huna malengo sijui tukuweke katika nafasi gani, katika maisha ya kila siku inabidi kujipangia mipango ambayo itasaidia kufikia kwa malengo yako, kama sasa mwaka unaenda kuisha naweza kukuuliza mwaka huu umepanga malengo gani na je umeyatimiza tayari?

Sio katika kazi tu unatakiwa kupanga malengo yako hata kwenye biashara na mipango ya familia pia unatakiwa kufanya hivyo, basi achana na hayo leo lengo letu ni moja tu, kukujuza jinsi ya kupanga malengo ukiwa kazini.

KWANZA: Pata calander ambazo unauhakika wa kutumia, na uandike kila kitu unachopaswa kufanya wakati unapoweka miadi au kuweka tarehe ya mwisho.

Calender ya mezani huweka mipango yako mbele yako wakati wote, lakini utandawazi umekuwa mkubwa sana siku hizi calander za kielektroniki zinaweza kubebeka na zinaweza kukupa taarifa muda wowote kupitia simu yako ya mkononi.

Tumia zote mbili ikiwa itasaidia, hakikisha tu kwamba umeweka notification on na ume-save matukio yako muhimu.

PILI: Safisha dawati lako kila jioni kabla ya kuondoka ofisini, uko katika nafasi nzuri zaidi ya kujua karatasi zinakwenda wapi na hapa tunamaanisaha kuwa malengo yanakuja na usafi usiache sehemu unayofanyia kazi kuwa chafu, pia usafi mwingine ni kuhusiana na kufanya kazi zako za siku hiyo zote usibakishe kiporo maana huwezi jua kesho utakuwa na majukumu gani.

TATU: Jenga tabia zinazoweka malengo na mpangilio wako sahihi, kwa mfano, ukiwa na kikombe chako cha kahawa asubuhi, kagua barua pepe zako zote, ufute ujumbe usio wa lazima na uangazie zile zinazohitaji jibu.

Fanya mazoea ya kuangalia calander yako kabla ya kuondoka nyumbani kila siku ili kuhakikisha kuwa una dhana zote muhimu unazohitaji kwa kazi iliyopangwa ya siku hiyo.

NNE: Tengeneza orodha. Unda orodha za kila siku na kila week na  uhakikishe zinakamilika.

 TANO: Chapisha maneno ya kutia moyo kwenye dawati lako, ukining'iniza kwenye ukuta wako na popote pengine itakusaidia kukumbunga malengo yako.

SITA: Panga matokeo bora katika ofisi yako ili kila atakaye kuja aweze kuona jinsi gani uko smart na unafanya kazi kwa bidii, hii itakusaidia hata wakati ukiacha kazi sehemu moja na kwenda kwingine watu kukupokea kwa ukubwa uliotoka nao katika kampuni uliyoacha kazi.

Kingine cha kuongezea ni kujitambua kuwa wewe ni nani, unafanya nini, upo kwa ajili gani hii itakusaidia kuacha kufanya kazi kwa mazoea, baadhi ya wafanyakazi wengi siku hizi wanafanya kazi kwa mazoea ambapo hii inawafanya mpaka wafukuzwe, jambo hili litakufanya usitimize malengo yako uliyojipangia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags