Namna ya kuendesha biashara kiakili

Namna ya kuendesha biashara kiakili

Say ayeyeee!! Ni bahati yako kukutana tena msomaji na mfuatiliaji wa kipengele cha Nipe Dili kila kukicha nikupeana madini mbalimbali yakuweza kutusaidia kufika tunapataka au sio?

Twende sawa sasa leo kwenye Nipe dili nakuletea mezani mchongo huu hapa njia zitakazokusaidia kuendesha biashara yako kisomi hivyo basi fuatilia dondoo hii.

  • Moja, Unatakiwa kuweka akilini mwako kuwa sio lazima mwenye biashara awe msomi.
  • Mbili, unatakiwa kutambua kuwa sio kila msomi anaweza kuendesha biashara kisomi.
  • Tatu, kuendesha biashara kisomi kunamfanyi mtu akafanikiwa na kupata faida katika biashara yake.
  • Nne, Unapaswa kufahamu kuwa kuendesha biashara kisomi ni zaidi ya elimu ya darasani ya biashara.

Nakufungulia ukurasa sasa, kuendesha biashara kisomi ni pale unapoamini na kutenda mambo yanayohusu biashara yako kwa imani na mtazamo kuwa ipo siku tu itakua na utapata faida.

Ili wewe ujinufaishe na upate faida kupitia hiyo biashara yako una budi kutambua mambo haya machache yafuatayo.

  • Itazame biashara yako kama mtoto ambaye amekwisha zaliwa anayehitaji kuishi kwa miaka mingi iwezekanavyo, unahitaji kuikuza, iyonekane yenye umuhimu, kuilinda dhidi ya majanga na pale inapokosa wateja au changamoto nyengine za wewe kama mzazi unatakiwa kuhakikisha inarudi kwenye hali yake ya awali.

Maelezo haya yanajidhilisha kupitia mfano huu hapa, kwani wapo wazazi wanaozaa watoto wakawatelekeza na wapo wanaowalwa watoto wao kwa shida na raha na mbeleni uja kuwasaidia hivyo kwenye biashara unatakiwa kuichukulia kama kiumbe.

  • Embu jiulize maswali yafuatayo kwanza

Biashara zote tunazosema zinaendeshwa kisomi ni kuwa zimejifafanua wazi kuwa zipo kutatua tatizo fulani, je zimejifafanua vyema namna gani zitatatua tatizo hilo, na vipi zinataka kujulikana ulimwenguni? Maelekezo haya kwenye biashara hutajwa katika mambo mawili Mission na Vision.

Note kwamba kupata faida sio dalili ya kuendesha biashara kisomi tambua hilo.

  • Biashara ya kisomi ina mipango ya kuifanya biashara iwe endelevu.

Mipango na mikakati mara kwa mara inafanywa ili kuifanya biashara iweze kujiendesha, kukua na isiwe tegemezi kwa maamuzi yasiyo ya kitaalamu.

Kufanya biashara endelevu ni pamoja na kuhakikisha biashara ina akiba ya kutosha na uongozi unaotambua thamani ya biashara.

  • Biashara ianyoendeshwa kisomi imemuweka mteja mbele.

Always mteja anakua kipaumbele ili biashara yako iendeshwe kisomi unatakiwa kupata muda mwingi wa kujifunza tabia, mahitaji na uwezo wa wateja katika kununua bidhaa.

Unatakiwa pia kujenga mahusiano bora na wateja ili uweze kufikia wengi zaidi na zaidi.

  • Biashara inayoendeshwa kisomi inazingatia kuwa na usimamizi ulio imara, hapa sasa kwenye ujuzi wa bidhaa husika inayozalishwa au kuuzwa pia ujuzi wa mambo ya msingi kama vile usimamizi wa fedha.

Usimamizi wa wafanyakazi, mawasiliano sanifu, ujuzi wa masoko , uwezo wa kuweka mipango, kodi na ujuzi wa kusoma mazingira na mabadiliko katika jamii ili kuweza kuendana na mabadiliko.

Note sio lazima mmiliki wa biashara ajue yote hayo ila anaweza kuajiri watu wenye ujuzi wa mambo husika wakamsaidia.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags