Naira Marley na Sam Larry waachiwa kwa dhamana

Naira Marley na Sam Larry waachiwa kwa dhamana

Baada ya kukaa kizuizini kwa wiki kadhaa hatimaye mwanamuziki #NairaMarley na ‘promota’ wake #SamLarry wameachiwa kwa dhamana ya N20 milioni ambayo ni zaidi ya tsh 61 milioni kwa kila mmoja.

Kwa mujibu wa Gossip Mill Nigeria imeeleza kuwa wawili hao walipewa dhamana hiyo huku kila mmoja akihitajika kuwasilisha passport zake za kusafiria za kimataifa huku wakipatiwa masharti ya kufika kila wiki katika Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Serikali (CID).

Aidha hakimu anayesimamia ‘kesi’ hiyo aliwapa onyo wawili hao kufuatia majaribio yoyote ya kuwasiliana na hakimu huyo kwa ajili ya kutaka rushwa yoyote ile yatarekodiwa na kutumika kama ushahidi mahakamani.

NairaMarley na SamLarry walikamatwa na jeshi la polisi mara tuu baada ya kurejea Nigeria kwa tuhuma za kifo cha mwanamuziki Mohbad kilichotoke Septemba 12 mwaka huu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags