Mzize kama Mayele

Mzize kama Mayele

‘Streika’ wa #Yanga Clement Mzize taratibu ameanza kufuata nyayo za mshambuliaji wa zamani wa ‘klabu’ hiyo Fiston Mayele ambaye ameondoka kwenye timu hiyo katika dirisha la usajili la hivi karibuni.

Mayele ambaye ni ‘streika’ namba tisa kama ilivyo Mzize alifunga kwenye michezo yote miwili ya ngao ya jamii katika misimu miwili aliyohudumu kwenye kikosi cha Yanga.

Wakati watu wanawaza jinsi pengo la Mayele litakavyozibika, Mzize ameonekana kuanza kuonyesha tabia za Mayele kwa kufunga kwenye mchezo wa ngao ya jamii kama alivyofanya siku ya jana kwenye ‘mechi’ dhidi ya Azam iliyopigwa Tanga ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mzize ambaye aliingia kipindi cha pili alifunga bao hilo dakika ya 89 kwa ‘shuti’ kali alilopiga nje ya ‘boksi’ la Azam.

Licha ya hivyo nyota huyu huenda asiwe mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza kwa sababu ya uwepo wa Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni ambaye amesajiliwa kuziba pengo la Mayele.

Mzize ni zao la ‘timu’ ya vijana ya Yanga na kisha akapandishwa kwenye kikosi cha wakubwa kwa msimu uliopita ambapo alifunga mabao 11 ya michuano yote, mitano kwenye ‘ligi’ na sita kwenye FA.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags