Mzava ajibu tuhuma za kumtapeli Kayumba sh 7 milioni

Mzava ajibu tuhuma za kumtapeli Kayumba sh 7 milioni

Muongozaji video, Erick Mzava amekanusha madai ya kumtapeli mwanamuzi Kayumba akisema amesharudisha sehemu ya fedha kiasi cha Shilingi 7 milioni ambazo alipewa kwa ajili ya kutengeneza video ya wimbo 'Shake' wa msanii huyo, iliyotoka Februari mwaka jana.

Hivi karibuni, Kayumba aliibua madai kuwa Mzava na mwanamuziki Rayvanny wamemtapeli kiasi hicho cha fedha ambacho alitoa kama malipo ya kufanyiwa kazi ya kuandaa video ya wimbo huo ulio katika albam yake ya 'Fine Tape'.

Mzava aliiambia Mwananchi kwa njia ya simu kuwa sakata hilo lilianza baada ya kazi waliyopanga kuifanya kushindwa kufanyika lakini tayari kuna kiasi cha fedha alisharudisha kwa Kayumba.

“Sikugoma kumpatia fedha hizo wala sikumwambia kuwa sitompatia kwani tayari nilishampatia milioni 5 ilibaki ni milioni mbili tu. Angenifuata au kunipigia simu tungezungumza na tungeyamaliza na siyo kwenda moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii, watu tunalipa kodi hadi Sh 8 milioni kwa mwezi nisingeshindwa kumpatia pesa yake,” amesema Mzava

Hata hivyo Mzava ameongezea kwa kueleza kuwa wasanii na mashabiki wapunguze chuki na wazidishe upendo ili kuendelea kusaidiana katika mambo mengine.

Mwananchi imefanya juhudi za kumtafuta Kayumba lakini hajapatikana. Endelea kufuatilia website yetu kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags