Mwizi akamatwa baada ya kujifanya mdoli kwenye duka la nguo

Mwizi akamatwa baada ya kujifanya mdoli kwenye duka la nguo

Kijana wa Kipoland mwenye umri wa miaka 22 ambaye hajafahamika jina lake anashikiliwa na polisi baada ya kubainika akijifanya mdoli (mannequin) wa kuwekea nguo dukani, kwa lengo la kuiba.

CCTV zilimnasa kijana huyo akiwa ameshikilia pochi mbele ya dirisha la duka la kioo akisubiri lifungwe ili aweze kuiba, ambapo maduka kadhaa yaliripoti kuibiwa pesa, nguo na vitu vya thamani.

Kwa mujibu wa Polisi wa Warsaw walieleza mbinu za kijana huyo kuwa huingia katika mgahawa na kula chakula cha kutosha kisha kununua nguo mpya na kuzivaa kwa ajili ya kujitayarisha kwenda kuiba, kitendo ambacho wamiliki na wafanyakazi wa maduka hawakugundua chochote

Polisi walimkamata kijana huyo baada ya kumfuatilia kwa muda matendo yake na kumpeleka katika kituo cha polisi huku ikidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo huenda akatumikia kifungo cha miaka 10.
.
.
.
#MwanananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags