Mwili wa O.J. Simpson kuchomwa moto

Mwili wa O.J. Simpson kuchomwa moto

Mwili wa aliyekuwa mwanamichezo wa zamani ambaye pia alikuwa mwigizaji kutoka nchini #Marekani O. J. Simpson utachomwa moto baada ya kukamilisha taratibu za shughuli za mazishi.

Imeripotiwa kuwa baada ya taratibu zote kufanyika mwili huo utachomwa moto kwa sababu ya kupoteza ushahidi wa ubongo wake kuchukuliwa na kutumika kwenye kituo maalum cha utafiti wa masuala ya ubongo ya CTE nchini humo.

Uchunguzi huo unakuja baada ya mwigizaji huyo kuwahi kushutumiwa kufanya mauaji mara mbili na ilidaiwa kuwa mauaji hayo aliyafanya akiwa na ugonjwa wa wasi wasi unafahamika kama CTE.

Kabla ya kifo chake Simpon aliwahi zungumzia kuhusu ugonjwa wake wa wasiwasi ambao uliathiri ubongo wake unaotokana na mishituko mingi aliyowahi kuipata wakati wa michezo.

O.J. Simpson alifariki dunia wiki iliyopita kwa tatizo la saratani ya tezi dume iliyogundulika miezi miwili iliyopita.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags