Mwili wa mwanasoka wa Bosnia wapatikana mtoni

Mwili wa mwanasoka wa Bosnia wapatikana mtoni

Mwili wa mcheza ‘soka’ kutoka nchini #Bosnia, #NedzadMujagic umepatikana kwenye mto baada ya ajali ya gari kuzama mtoni na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi watatu usiku wa jana.

Mujagic ambaye alikuwa nahodha wa ‘timu’ ya #Sloga nchini humo alipoteza maisha pamoja na ‘kocha’ msaidizi #AdnanFajic katika mto #Una kwenye kisiwa cha #Bosanka.

Hata hivyo mpaka sasa gari iliyohusika kwenye ajali hiyo imetolewa mtoni lakini mwili wa ‘kocha’ msaidizi Adnan bado haujapatikana.

Walionusurika ni wachezaji watatu wa 'timu' ya Sloga, ambao walifanikiwa kuogelea na kujiokoa.

Sloga ni 'timu' inayocheza kwenye daraja la pili katika soka la Bosnia, 'klabu' hiyo ilianzishwa mwaka 1922 ni moja kati ya klabu zenye historia kubwa nchini humo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags