Mwigizaji wa Bongo Movie kortini adaiwa kuiba 4.6 milioni

Mwigizaji wa Bongo Movie kortini adaiwa kuiba 4.6 milioni

Msanii wa zamani wa Kaole na mwigizaji wa filamu nchini, Dorah Mwakatete maarufu kama Kadadaa, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo, Dar es Salaam na kusomewa shtaka moja la wizi wa Sh4.6 milioni.

Kadadaa ambaye aliwahi kuwika katika uigizaji miaka ya 2000 akiwa na kundi la Kaole, amefikishwa mahakamani hapo leo, Julai 19, 2024 na kusomewa shtaka hilo na karani Aurelia Bahati, mbele ya Hakimu Gladnes Njau.

Bahati amedai kuwa Kadadaa alitenda kosa hilo Juni 26, 2023 saa 10:00 alasiri katika jengo la PSSSF Tower, Mtaa wa Samora lililopo wilaya ya Ilala.

Alidai siku hiyo ya tukio, mshtakiwa aliiba Sh4,658,000 mali ya Feisal Sonzera huku akijua kitendo hicho ni kosa kisheria.

Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka hilo amekana kutenda kosa hilo na kuomba apatiwe dhamana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags