Mwigizaji Majors, Akwepa kwenda jela

Mwigizaji Majors, Akwepa kwenda jela

Mwigizaji kutoka nchini Marekani Jonathan Majors (34) amekwepa kwenda jela mwaka mmoja na kukubali kupatiwa ushauri nasaha kuhusiana na unyanyasaji wa nyumbani, hii ni baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga na kumnyanyasa aliyekuwa mpenzi wake Grace Jabbari.

Hukumu hiyo iliyotolewa Jumatatu, April 8, katika mahakama ya juu ya Manhattan na jaji Michael Gaffey ilieleza kuwa Majors amehukumiwa kutokana na makossa mawili ambayo ni kumshambulia Grace kwa kukusudia na kumfanyia unyanysaji wa nyumbani wakati walipokuwa wakiishi pamoja.

Kwa mujibu wa waendesha mashitaka Majors alitakuwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela lakini kutokana na kuendelea na matibabu ya afya ya akili wamependekeza kupatiwa ushauri nasaha ndani ya mwaka mmoja kuhusiana na unyanyasaji.

Ikumbukwe kuwa tukio hilo limedaiwa kutokea Machi 2023 katika gari la SUV jijini Manhattan ambapo mwanamke huyo ameeleza kuwa amefungua shitaka hilo kwa ajili ya kudai fidia kutokana na majeraha aliyoyapata.

Jonathan Majors amejizolea umaarufu kupitia filamu zake kama ‘Devotion’, ‘Ant-Man and the Wasp: Quantumania’, ‘Creed III’, pia anatarajiwa kuonekana katika filamu ya ‘Avengers: The Kang Dynasty’ inayotarajia kutoka mwaka 2026.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags