Mwenyekiti wa bodi Simba, Kwenye picha ya pamoja na  Rais wa Fifa

Mwenyekiti wa bodi Simba, Kwenye picha ya pamoja na Rais wa Fifa

“Nimefurahi kukutana na Rais wa FIFA, Gianni Infantino pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu wa FIFA, Ornella Desirée Bellia kujadili kuhusu Super League hapa Park Hyatt jijini Sydney, Australia.

Majadiliano yamekuwa mazuri na jambo jema Rais Infantino anaielewa vizuri Tanzania na ameniahidi atakuwepo kwenye uzinduzi wa Super League ambao utafanyika Tanzania. Tumezungumza mazuri mengi ambayo yatakuja nyumbani Tanzania kwa ajili ya mpira wa miguu.

Tuko hapa Sydney kushiriki ‘kozi’ ya Diploma katika Uongozi wa ‘Klabu’ inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) lakini pia kufanya shughuli za mpira ikiwepo kujifunza namna mashindano makubwa yanaandaliwa kama Kombe la Dunia la Wanawake ambalo linafanyika hapa Australia na New Zealand.

Kama mnavyofahamu Simba itashiriki katika Africa Super League hivyo uzoefu huu utatusaidia katika uandaaji wa sherehe za ufunguzi pamoja na michezo ya kimataifa iliyopo mbele yetu”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags