Mwandishi wa habari maarufu na mkosoaji wa serikali ya Senegal ambaye amekuwa kwenye mgomo wa kula kupinga mashtaka dhidi yake amehamishiwa hospitalini baada ya afya yake kuzorota.
Wakili wa Pape Ale Niang ambae ni mkuu wa tovuti ya habari ya mtandaoni ya Dakar Matin, amesema aligoma kula mnamo Desemba 2 baada ya kuwa kizuizini kwa wiki kadhaa na baadae alilazwa hospitali na kuachiliwa kwa muda kabla ya kukamatwa tena Decemba 20.
Aidha mwandishi huyo alikamatwa Novemba 6 na kushtakiwa kwa kufichua habari zinazoweza kuhatarisha usalama wa taifa.Kesi dhidi yake iliibuka baada ya kuandika kuhusu mashtaka ya ubakaji yanayomkabili kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Ousmane Sonko.
Leave a Reply