Mwanaume aliyepandikizwa moyo wa nguruwe afariki

Mwanaume aliyepandikizwa moyo wa nguruwe afariki

Baada ya mtu wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa kupandikizwa moyo wa nguruwe mwaka jana na ‘timu’ ya madaktari kutoka Chuo Kikuu Maryland kufariki miezi miwili baada ya upasuaji huo, mtu wa pili kufanyiwa upandikizi huo naye afariki dunia.

Mtu huyo anayefahamika kwa jina la Lawrence Faucette, alifariki dunia baada ya kupandikiziwa moyo huo ikiwa ni wiki sita tuu tangu upasuaji huo ufanyike.

Kwa mujibu wa BBC inaripoti kuwa Chuo Kikuu cha Maryland Medical Center, ambapo utaratibu wa majaribio ulifanyika,kilisema moyo ulianza kuonesha dalili za kutokufanya kazi katika siku za hivi karibuni.

Mwezi mmoja baada ya upasuaji wake, madaktari wake walisema wanaamini kuwa moyo wake ulifanya kazi vizuri na waliondoa dawa zote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags