Mwanaume aliyefuga nywele miaka mitatu, amtengenezee wigi mpenzi wake

Mwanaume aliyefuga nywele miaka mitatu, amtengenezee wigi mpenzi wake


Katika hali ya upendo usiyo wa kawaida mwanaume anayefahamika kwa jina la Cody Ennis, alifuga nywele zake kwa muda wa miaka mitatu kwa lengo la kumtengenezea wigi mpenzi wake aitwaye Hannah Hosking.

Mwanaume huyo alichuka uamuzi huo kutokana na ugonjwa wa alopecia, unaomsumbua mpenzi wake na kumpelekea nywele zake kunyonyoka. Inaelezwa kuwa wawili hao walipokutana mara ya kwanza, Hana alikuwa akivaa mawigi tu kutokana na kutokuwa na nywele lakini miezi sita baada ya kuchumbiana, mwanaume wake alijitolea kukuza nywele zake kwa lengo la kumtengenezea mpenzi wake wigi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Inspiring News inaeleza kuwa ili kuhakikisha nywele hizo zina ubora mwanaume huyo alitumia vitu mbalimbali kama vile mafuta na shampoo ili kuzifanya zikue vizui bila kukatika.

Hata hivyo Oktoba 2023 ikiwa ni baada ya miaka mitatu, nywele zikiwa zimefikia inchi 29, Cody alizikata, na kisha kuzipeleka kwa mtengenezaji wa wigi anayeitwa Florida Fancies ambaye alikamilisha kutengeneza wigi hilo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post