Mwanaume akimbia baada ya mpenzi wake kuwa na ujauzito wa watoto watatu

Mwanaume akimbia baada ya mpenzi wake kuwa na ujauzito wa watoto watatu

Mwanamke mmoja kutoka nchini Nigeria mwenye umri wa miaka 27 anayetambulika kwa jina la Marry, adai kukimbiwa na mpenzi wake baada ya kumwambia kuwa anaujauzito na anatarajia kupata watoto watatu.

Mwanamke huyo amefunguka kuhusu masaibu hayo anasema walipanga kufunga ndoa na mpenzi wake huyo kabla ya kuondoka kisa ujauzito wa watoto watatu.

Aliendelea kueleza kuwa mwanaume huyo alienda kuwaona wazazi wake kwa ajili ya kuomba ruhusa ya kumuoa Marry lakini baada ya kumpa ujauzito alitokomea mahali pasipo julikana.

Sasa akiwa na watoto hao wachanga watatu, Mary amedai yeye na wanawe wanaishi kwa huruma ya mwenyenyumba. Alifichua kuwa awali alifanya kazi ya kushona nguo lakini ujauzito ulimfanya adhoofike, na alishindwa kuendelea na shughuli hiyo.

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags