Mwanasheria anayeishi kwa kupumulia mashine ya mapafu kwa zaidi ya miaka 70

Mwanasheria anayeishi kwa kupumulia mashine ya mapafu kwa zaidi ya miaka 70

Waliosema kabla hujafa hujaumbika wala hawakukosea, kwa sababu wapo watu wengi tunawafahamu walikuwa wazima lakini sasa hawana baadhi ya viungo, huku wengine wakiwa kitandani hawawezi kufanya kitu chochote.

Leo hii mfahamu mwanaume mmoja kutoka nchini Marekani anayefahamika kwa jila la Paul Alexander, wenye umri wa miaka 77 amevunja record ya kuishi zaidi miaka 70 kwenye pafu la chuma.

Paul aliugua Polio akiwa na umri wa miaka 6 mwaka 1952 ambao ugonjwa huo ulimpelekea kupooza na mapafu yake kuharibika hivyo hulazimaki kutumia kifaa cha chuma kwaajili ya upumuaji (Iron Lung).

 Licha ya wengi kutokuwa na imani kama ataishi muda mrefu, lakini Paul hakukata tamaa ndipo mwaka 2020 aliandika kitabu, kilichoelezea maisha yake kwenye mapafu ya chuma, haikuwa rahisi kwani alitumia miaka mitano hadi kukamilisha kitabu hicho, na kila neno aliliandika yeye mwenyewe bila kutegemea usaidizi wa mtu.

Kifaa alichotumia kuandikia kitabu hicho ni kalamu iliyounganishwa kwenye fimbo, na alitumia mdomo kushika kalamu hiyo wakati wa kuandika kitabu, hadi sasa amepata mafanikio kwa kuhitimu shule ya sheria na kua wakili.

Katika mahojiano yake na mmoja ya chombo cha habari nchini humo alieleza kuwa ameishi maisha kamili na ya kusisimua hakukata tamaa.

“Nilibuni njia ya kupata hewa na kupumua, niliifanyia kazi kwa mwaka mmoja kabla ya kufikia dakika hizo tatu, lakini nilifanikiwa na kuvunja record”

Hatimaye kupitia zoezi hilo Alexander anaweza kuvuta hewa kwa muda fulani, na kisha kuondolewa kwenye mashine hiyo kwa muda mchache, ingawa sio rahisi yeye amefanikiwa kuwa  mtu wa kwanza mwenye tatizo hilo kufanya hivyo.

Kati ya vitu ambavyo Paul, anakili kutofanya kwenye maisha yake ni kutumia ulemavu wake kama sababu ya kutia huruma au kushindwa kufanya kazi  kwa sababu bado anandoto kubwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags