Mwanariadha wa Kenya atunukia cheti na Guinness

Mwanariadha wa Kenya atunukia cheti na Guinness

Mwanariadha kutoka nchini Kenya aitwaye Peres Jepchirchir amevunja rekodi ya dunia ya ‘Guinness World Record’ kwa upande wa wanawake kwa kukimbia mbio ndefu za London Marathon 2024, akitumia saa 2:16:16 na kuipiku rekodi ya awali ya Mary Keitany kwa sekunde 46.

Hatua hiyo ilipelekea Peres kuingia katika kitabu cha rekodi ya dunia cha ‘Guinness World Record’ ambapo shirika hilo lilimkabidhi mwanadada huyo cheti maalumu cha kuvunja rekodi.

Japo Peres hatopatiwa zawadi ya pesa kutoka Guinness World Records, kama ilivyo kawaida kwa wavunjaji rekodi lakini atapokea zawadi ya ushindi kutoka Landon Marathon, ambayo ni kiasi cha dola 55,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 142 milioni.

Washindi wengine wa rekodi ya dunia ni Tigst Assefa, Megertu Alemu wa Ethiopia, na Mkenya Joyciline Jepkosgei ambapo Tigst Assefa wa Ethiopia alikuwa wa pili huku Joyciline Jepkosgei wa Kenya akiwa wa tatu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post