Mwanariadha Pistorious kuachiwa huru leo

Mwanariadha Pistorious kuachiwa huru leo

Ulimwengu wa wapenda michezo baadaye utashuhudia tukio la kuachiwa huru kutoka gerezani mwanariadha wa zamani wa mbio fupi, Oscar Pistorious, raia wa Afrika Kusini.

Nyota huyu anaachiwa huru baada ya kutumikia kifungo kwa miaka isiyopungua tisa, na sasa ataenda kutumikia kifungo cha nje hadi mwaka 2029.

Oscar (37), alihukumiwa kifungo cha miaka 13 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi mara nne.

Alimuua Reeva aliyekuwa ameingia ndani kwake wakati Oscar akiwa bafuni. Katika utetezi wake, nyota huyo alisema alifyatua risasi ikiwa ni sehemu ya kujihami kwani alidhani ni mwizi ameingia nyumbani kwake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags