Mwanariadha Kenya afariki dunia

Mwanariadha Kenya afariki dunia

Mwanariadha wa mbio ndefu kutoka nchini Kenya, Kelvin Kiptum na ‘kocha’ wake raia wa Rwanda, Garvais Hakizimana wamefariki dunia kwa ajali ya gari, jana Jumapili katika eneo la Kaptagat nchini humo.

Inaelezwa gari hiyo aina ya Toyota iliyokuwa ikiendeshwa na Kiptum ilikuwa na jumla ya watu watatu akiwemo mwanamke mmoja, ilipoteza muelekeo na kwenda kugonga mti mkubwa.

 Hata hivyo katika ajali hiyo Kiptum na kocha wake walifariki dunia huku mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Sharon Kosgey akikimbizwa hospitali kutokana na majeraha aliyopata.

Kiptum amefariki akiwa na umri wa miaka 24 aliwahi kushinda tuzo tatu ikiwemo ‘World Marathon Majors’ (WMM), zilizofanyika Desemba 2022 na Oktoba 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post