Mwanamke na uongozi chuoni

Mwanamke na uongozi chuoni

Na Michael Anderson
Wanawake chuoni wanahitajika kuaminisha jamii ya kwamba kila mwanamke ana uwezo mkubwa ndani yake, kila mwanamke ana hatima kubwa inayomsubiri, kila mwanamke anaweza kubadilisha historia yake na kuacha alama kubwa.

Hata hivyo wanawake wengi sana wanaishi katika hali ya kutokujiamini, kudharauliwa na wengi wapo katika maumivu makali ya moyo yaliyotokana na changamoto mbalimbali walizowahi kuzipitia ama ambazo wanazipita kwa sasa katika maisha yao.

Wapo wanawake wengi ambao wameshakata tamaa kuhusiana na maisha yao ya kusoma, kuna wengine hawataki kujaribu tena na kuna wengine ambao waliwahi kujaribu kujitoa uhai wao kwa sababu ya changamoto za maisha vyuoni kama kuambukizwa virusi vya UKIMWI chuoni, kufeli masomo chuoni, kukosa msaada wa kifamilia pindi wapo masomoni,mimba zisizo za kutarajia ambazo hupelekea kukata tamaa na maisha ya chuo na maisha ya uongozi ambapo pengine ungesaidia chuo ,jamii yake ama taifa kwa ujumla

CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA KATIKA NYANJA YA UONGOZI

(i) kushuka kwa imani kwa viongozi wa kike.
Novemba, data mpya kutoka katika Reykjavik Index, utafiti wa mwaka ambao unalinganisha jinsi wanaume na wanawake wanavyotazamwa inapokuja katika suala la kufaa kwao katika nafasi za mamlaka, zilionesha kuwa imani kwa viongozi wanawake imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi chote cha mwaka hivyo katika sekta ya elimu vyuoni imani inapungua kwa wanawake kutokana na waliotangulia kupewa nafasi wanashindwa kuwajibika vyema katika nafasi zao inapelekea kutokuaminiwa kwa wanawake vyuoni

(ii) suala la rushwa ya ngono .
Hili limekua ni tatizo kubwa haswa katika kupata nafasi za uongozi chuoni, mara kadhaa imeonekana wanawake wengi wanapania nafasi za juu kama urais wa chuo ama makamu wa rais tume za uchaguzi zinahusishwa sana kupokea rushwa ya ngono ili kuwapitisha wanawake kugombea nafasi hizo za juu za uongozi katika serikali za wanafunzi.

(iii) Suala la uchumi na fedha
Kama inavyofahamika kupata nafasi ni mchakato ambao unahusisha sana fedha kuanzia uchukuaji wa form mpaka kampeni wanawake wengi chuoni wanakubwa na changamoto hii na muda mwingine kukosa wanaowaamini kuwekeza pesa zao kwa viongozi wa kike hivyo wanakosa sapoti ya kutosha kutoka kwa marafiki na viongozi waliowatangulia .


NINI KIFANYIKE ILI KUEPUKANA NA CHANGAMOTO HIZO

(i)Jiamini na amini unachokifanya acha tamaa
Acha tamaa na nafasi ambazo huna uzoefu nazo ,huna malengo nayo uongozi siyo sehemu ya mzaha uongozi chuoni ni kufika katika maisha ya watu kugusa maisha ya walio wengi fanya ambacho ni sahihi kwa maslahi ya walio wengi na hiyo itakufanya kuwa wa thamani na ubora.

(ii) Epuka kuwa mwepesi kwenye maamuzi
Kabla ya kuamua kuchukua form ama kujitosa katika nafasi fulani epuka kuchukua maamuzi kwa haraka fika kwa watu waliokutangulia na kukuzidi waelezee desire za ndani yako juu ya suala zima la uongozi then fanya maamuzi ambayo hayahusishwi na mikumbo itakusaidia

(iii)Amini unaweza na uwezo wako binafsi hauwezi kukusaliti
Wanawake wengi ni wasomi wazuri na wanauwezo wa kufanya kazi nzuri katika nafasi walizoaminiwa lakini kwa kutojiamini kuongoza hukubali waongozwe na wanaume.

Wapo wanawake wanaambiwa tunakupa nafasi hii wanaogopa kuchukua ile nafasi ukimuuliza sababu anasema mimi siwezi, unamuuliza mbona umesoma kushika nafasi hiyo hakubali.

Wanawake wanaweza kupata hizo nafasi lakini wakawa tayari kufanya kazi kwa kusaidia kiongozi mwanaume ambaye ana kiwango cha elimu na yeye lakini kuchukua nafasi hiyo ya uongozi hayupo tayari kufanya kwani kundi hilo limekuwa nyuma sana katika mambo mengi na hata katika kufanya maamuzi hivyo wewe msomi mwanamke usikubali kuukana uwezo wako.

Kwa sasa hapa nchini kuna ongezeko la idadi ya viongozi wanawake bungeni, taasisi za umma na katika ngazi mbalimbali za utawala serikalini tunapongeza wanawake majasiri ambao wanaonesha umahiri mkubwa na ujasiri katika kufanya maamuzi yanayohusu taifa, familia na jamii inayowazunguka pamoja na changamoto nyingi za kijinsia, kifamilia, kiuchimi na kihisia zinazowazunguka tofauti na wanaume.

Hakika mwanamke akiwa katika kiti cha maamuzi basi ni rahisi kuundwa sera, mikakati na mipango inayowanu-faisha wanawake wengi zaidi na mwanamke akifanikiwa kiafya, kielimu na kiuchumi basi jamii na taifa kwa ujumla litakuwa limefanikiwa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags