Mwanamitindo aliyewahi kumvalisha Jennifer Lopez afariki dunia

Mwanamitindo aliyewahi kumvalisha Jennifer Lopez afariki dunia

Aliyekuwa mwanamitindo maarufu nchini Italia, #RobertoCavalli mwenye umri wa miaka 83 maarufu kama ‘King of leopard print’ amefariki dunia jana Jumamosi.

Cavalli ambaye alikuwa akisumbuwa na maradhi kwa muda mrefu amekutwa na umauti akiwa nyumbani kwake katika mji wa Florence nchini humo.

Ubunifu wake umevaliwa na watu mbalimbali mashuhuri akiwemo Jennifer Lopez, Beyonce, Kim Kardashian, Naomi Campbell na wengine wengi.

Ikumbukwe kuwa mwaka 1970 aliwahi kufungua kampuni na alianzisha lebo yake ya kuuza nguo za kifahari, pochi, viatu na manukato.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags