Mwanamieleka Virgil afariki dunia

Mwanamieleka Virgil afariki dunia

Mwanamieleka kutoka nchini Marekani, Michael Jones ‘Virgil’ afariki dunia akiwa na umri wa miaka 61 baada ya kusumbuliwa kwa ugonjwa wa saratani ya utumbo kwa muda mrefu.

Taarifa ya kifo cha mwanamieleka huyo kimethibitishwa na refa wa Mieleka Mark Charles kupitia ukurasa wa X (zamani twitter) ambapo ameeleza kuwa Virgil alifariki akiwa hospitali wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Virgil alijulikana zaidi kati ya mwaka 1980 na 1990 kufuatiwa na umahiri wake katika mchezo huo ambao ulimfanya akubalike zaidi na Shirikisho la Mieleka duniani (WWF).

Mwanamieleka huyo mwaka 2022 alitangaza kusumbuliwa na tatizo la ubongo unaoathiri kumbukumbu na uwezo wa kufikiri pamoja na saratani ya utumbo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags