Mwanahawa Ally rasmi kuacha  muziki, maradhi yatajwa

Mwanahawa Ally rasmi kuacha muziki, maradhi yatajwa

Msanii mkongwe wa Taarab nchini Tanzania, Mwanahawa Ally, ameamua kuacha kuimba kutokana na maradhi yanayomsumbua.

Hayo yamebainishwa  na Zamaradi Mketema wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Zamaradi amesema kutokana na mchango wa Mwanahawa kwenye tasnia ya muziki wameamua kuandaa tamasha maalumu lenye jina la 'Asante Mwanahawa' kwa ajili ya kuwaaga mashabiki.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 28, 2024 katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, ambapo msanii huyo atawaaga rasmi mashabiki wake na kupumzika katika tasnia hiyo baada Rais Samia Suluhu Hassan kusikia kilio chake.

"Mwanahawa hivi karibuni aliwahi kufanya mahojiano na Zamaradi TV na kuelezea hali ngumu ya maisha anayokumbana nayo ikiwa pamoja na maradhi ya hapa na pale, na akaomba kukutana na Rais Samia Suluhu kwa ajili ya kutaka kupata msaada.

"Uzuri ujumbe ulifika na akapata msaada wa Sh10 milioni ambazo Rais alimtuma mtoto wake ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu kutokea Zanzibar, Wanu Hafidh Ameir ampelekee," amesema Zamaradi.

Msanii huyo ambaye alianza kazi ya sanaa mwaka 1966, amewahi kutamba na nyimbo kama Mwanamke Hulka, Mwenye Wivu Ajinyonge, Roho Mbaya Haijengi akiwa na kundi la Jahazi Modern Taarabu na nyinginezo nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags