Mwana FA: Mashabiki wajenge utamaduni wa kushangilia muda wote

Mwana FA: Mashabiki wajenge utamaduni wa kushangilia muda wote

Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwijuma maarufu kama #MwanaFA amewataka mashabiki wa ‘timu’ za mpira wa miguu kuacha kushangilia mabao tu kwani inawavunja moyo wachezaji wakiwa uwanjani.

Akizungumza katika mkutano wa ‘klabu’ ya #Yanga uliofanyika makao makuu ya ‘klabu’ hiyo Jangwani leo, Mwana-FA amesema mashabiki wamekuwa na tabia ya kushangilia matukio tu hivyo amewashauri wajifunze kujenga utamaduni wa kushangilia muda wote wa mchezo kwa sababu itasaidia mchezo kuwa mzuri.

Hata hivyo FA amewatakia kila la heri ‘klabu’ hiyo huku akiamini watarudi na matokeo mazuri katika mchezo wao wa marudiano ya nusu fainali ya ‘klabu’ bingwa Afrika utakao fanyika nchini Afrika Kusini siku ya Ijumaa, April 5.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags