Mwana FA: Kung’oa viti uwanjani ni uhuni kama uhuni mwingine

Mwana FA: Kung’oa viti uwanjani ni uhuni kama uhuni mwingine

Naibu Waziri, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa kung’oa viti uwanjani ni uhuni kama uhuni mwingine na wanaofanya uharibifu huo watachukuliwa hatua.

Ameyasema hayo baada ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya ‘klabu’ ya #Yanga na #Alahly, uliochezwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam, ambapo baadhi ya wachezaji wa ‘klabu’ ya Yanga wanadaiwa kung’oa viti baada ya mchezo huo ulioisha kwa sare ya bao moja.

Hata hivyo Waziri huyo amewahakikishia Watanzania kuwa waliofanya uharibifu kwenye mchezo huo wa ‘klabu’ bingwa Afrika (CAFL) watachukuliwa hatua kama walivyochukukuliwa hatua waliofanya uharibifu mwaka 2016 kwenye mchezo wa derby kati ya Simba na Yanga nao ulio malizika kwa sare ya 1-1.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags