Mwalimu azichapa na mwanafunzi wake.

Mwalimu azichapa na mwanafunzi wake.

Ebanaee!! Ugomvi wa mwalimu na mwanafunzi hivi inakuaje, hii sasa huko North carolia nchini Marekani katika shuke ya Rocky Mount walizichapa mwalimu na mwanafunzi.

Basi bana tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika Shule hiyo baada ya mwalimu Xaviera Steel kumpokonya mwanafunzi mmoja simu alipokuwa akiitumia darasani lakini mwanafunzi huyo alimrukia mwalimu hali ambayo ilichochea ugomvi mkubwa kati ya wawili hao.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari mbali mbali huko Marekani, Xaviera ambaye alikuwa kama mwalimu mbadala katika shule hiyo, inasemekana alimpokonya mwanafunzi huyo simu alipokuwa akiitumia darasani.

 Jambo ambalo mwanafunzi huyo  hakufurahishwa na kitendo hicho cha kupokonywa simu alimkaripia mwalimu wake akitaka amrejeshee simu yake akisema kuwa sheria hazitumiki kwa kila mtu na kusisitiza kwamba amrudishie simu yake.

"Kwa nini sheria hazitumiki kwa kila mtu mwingine. Hiyo ni simu yangu,” mwanafunzi huyo alisikika akisema. Mwalimu alimjibu kuwa sheria hizo zinatumika kwa kila mtu, huku akimwonya mwanafunzi huyo kutomgusa.

Lakini pamoja na hayo mwanafunzi huyo alimrukia hali ambayo ilichochea ugomvi huo kati ya wawili hao kwa kuingiana mwilini.

Sambamba na hayo Polisi wa Rocky Mount walithibitisha tukio hilo na kusema hakuna alie jeruhiwa lakini mwanafunzi amekiuka sharia akiwa amefanya kosa la kutumia simu darasani na kupigana na mwalimu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags