Mwaliko wa harusi wasuluhisha ugomvi wa Davido na Pinnck

Mwaliko wa harusi wasuluhisha ugomvi wa Davido na Pinnck

Mwamuziki kutoka nchini Nigeria #Davido amemwalika harusi yake aliyekuwa Rais wa shirikisho la Soka la Nigeria, NFF #AmajuPinnick ingawa walikuwa katika mzozo wa kisheria.

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo maarufu wa miondoko ya #Afrobeat ameonekana kusuluhisha kwa siri mzozo wake wa kisheria na Pinnick baada ya hivi karibuni Davido na mkewe, Chioma kwenda nyumbani kwa Pinnick kwa lengo la kumpatia mualiko wa harusi yao inayotarajiwa kufungwa hivi karibuni.

Utakumbuka kwamba Oktoba 31 mwaka 2023 Pinnck aliwasilisha kesi ya ukiukaji wa mkataba wa Naira 2.3 bilioni dhidi ya mwimbaji huyo, baada ya kushindwa kutumbuiza katika toleo la 19 la tukio la 'Warri Again' Oktoba 6, 2023.

Hata hivyo  kupitia mtandao wa Tiktok mke wa Pinnick, #JuliePinnick, alisisitiza nguvu ya upendo katika kukuza upatanisho na kuthibitisha kwamba walipokea mwaliko huo.

“David na Chioma walikuja nyumbani kwetu ili kuialika familia yangu kibinafsi kwenye sherehe ya ndoa yao. Nilifurahi kukutana na Chioma kwa mara ya kwanza; ni msichana mzuri sana, wacha upendo uongoze. tunamtakia Davido na Chioma maisha marefu ya siku zijazo pamoja milele.” Ameandika

Wiki mbili zilizo pita Davido alitangaza kuwa yeye na Chioma watafunga ndoa yao Juni 25, mwaka huu mjini Lagos nchini Nigeria.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags