Mwakinyo afungiwa kushiriki ngumi

Mwakinyo afungiwa kushiriki ngumi

Bondia maarufu nchini Hassani Mwakinyo amefungiwa kupanda ulingoni kwa muda wa mwaka mmoja na faini ya tsh 1 milioni kufuatia utovu wa nidhamu wa kugomea kupanda ulingoni.

Mwakinyo amefungiwa na Kamisheni ya Mchezo wa Ngumi Nchini (TPBRC) kwa kosa la kutopanda ulingoni katika pambano lililoandaliwa na Paff Promotion Septemba 29, mwaka huu lililofanyika Ubungo Plaza.

Katibu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) George Silas ameweka wazi maamuzi yaliyofanywa na kamati ya nidhamu na kushirikisha pande zote mbili ambapo ni uongozi wa Paff promotion wakiwa pamoja na Mwakinyo na kubaini kuwa changamoto zilikuwa ni kwa kwa Mwakinyo kutokuheshimu mkataba wa promota.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa bondia huyo ameandika ujumbe usemao “Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu nia ovu, pamoja na dhamira zenu mbaya na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa.

Nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi hadharani kwenye ili inapotokea tena issue kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu ni, kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu asiyejua thamani na haki zake za msingi”
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags