Mwaka wa kwanza chuoni

Mwaka wa kwanza chuoni

Na Magreth Bavuma

Niaje niaje wakuu karibuni tena kwenye ‘kona’ yetu pendwa ya wanavyuo “unicorner” eneo moja tu linalowakutanisha wajanja wote walioko vyuoni, na kama ni mara yako ya kwanza kujiunga na sisi jisikie uko nyumbani kabisa maana katika vitu tunajivunia ni hii familia kukua zaidi sasa twenzetu!!!!!!!!!

Kuingia chuo kikuu ni moja ya hatua muhimu katika maisha ya mwanafunzi. Ni wakati wa kupata elimu ya juu, kukua kibinafsi na kitaaluma, na kujiandaa kwa maisha ya baadaye, ukisema umuulize mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari moja ya ndoto atakazosema ni kufika chuo kikuu, na ukweli ni kwamba furaha ya kuchaguliwa kujiunga na chuo huwa haielezeki bhana.

“Chuo mbona bata” hili ndiyo neno ambalo baadhi hulitilia maanani sana wakati wa kujiandaa kujiunga na vyuo walivyochaguliwa, na kuna muda unakumbuka tu kwamba aah me si naenda chuo nitakua huru nitafanya chochote ninachojisikia. Ukipiga mahesabu yako wewe na marafiki zako tayari mnakua mmejipanga like “it’s us against the world”.

Hata hivyo, uhalisia wa maisha ya chuo ni tofauti na story zilizoko mtaani, katika kipindi hiki ambacho wadogo zetu wanajiandaa kujiunga na vyuo ni vizuri kuwaeleza ukweli wa uhalisia wa mambo yaliyopo vyuoni ili mwisho wa siku mtu asiseme hakuambiwa, ni heri ukweli unaouma kuliko uongo wa muda ambao matokeo yake yanaweza kuleta maumivu makubwa sana siyo kwa familia tu bali na jamii kwa ujumla ambayo inategemea wasomi ndiyo wasimame kama mfano wa kuigwa.

Kuwa mwaka wa kwanza nikama unakua punching bag ya watu, kila mtu atajifanya yuko more experienced than you which some of them might be right, lakini kuna wale wa kutaka ku-take advantage of you being a newbie in town na hao ndiyo wa kuwa nao makini sana, lakini pia kuna wale wenzangu na mimi umetoka zako mkoani na kwa mara ya kwanza unakanyaga town na kuja chuo kwa hiyo kila kitu kwako ni kipya kabisa.

Kuna mambo kadhaa ambayo uwezekano wa kukutana nayo kama first year ni mkubwa sana na baadhi yake ni kama vile,

Kuondoka nyumbani, wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza wanaondoka nyumbani kwa mara ya kwanza ili kwenda chuo kikuu. Hii inakuaje changamoto?  Wanafunzi wengine wanatoka fresh from school hivyo wanahitaji kujifunza jinsi ya kujitegemea na kuishi peke yao ambapo kutokana na kukosa experience ya kujitegemea kwao inakua changamoto sana.

Kuyaona masomo magumu, masomo ya chuo kikuu mara nyingi huwa magumu zaidi kuliko masomo ya shule ya sekondari na advance. Wanafunzi wanaweza kulazimika kusoma kwa bidii zaidi ili kupata mafanikio.

Vilevile wanafunzi wa chuo kikuu wanapaswa kujifunza jinsi ya kuchanganya masomo yao na shughuli zingine, kama vile kazi, michezo, na maisha ya kijamii ili kuepuka muingiliano unaoweza kusababisha usitimize malengo yako ya kuwepo chuoni.Lakini pia wanafunzi wa chuo kikuu wanaweza kukabiliana na pressure kutoka kwa jamii inayowazunguka na kusababisha kuishi kwa matarajio ya wengine na kupoteza focus ya kile wanachotaka wao kufanya.

Licha ya changamoto zake, maisha ya chuo kikuu pia yana fursa nyingi ambazo zinaweza kumuwezesha mwanafunzi, kukua kibinafsi na kitaaluma, kujiandaa kwa maisha ya baadaye kupitia fursa mbalimbali ambazo mwanafunzi anakutana nazo anapokua chuoni.

Sasa kuna mambo ya kuzingatia ili kama mwaka wa kwanza usiingie chuoni kinyonge wala kuwapa watu nafasi ya kuwa wasemaji wakuu wa maisha yako.

Kwanza kabisa hakikisha unajua ni nini unataka, kuwa na focus kwenye maisha yako ni muhimu sana ili kuepusha kufanya kitu ambacho kila mtu anakifanya nanukuu maneno ya mshindi wa taji la miss Tanzania 2023 Miss Tracy Nabukeera aliyoyasema kwenye moja interview aliyofanya mwanzoni mwa wiki hii “The same boiling water that can turn an egg hard can turn a potato soft so you have to make sure that in every environment that you are in you detect the environment and don’t let the environment dictate you”.

Jifunze kusema hapana, siyo lazima utumie nguvu kufanya vitu ambavyo yamkini huko nyuma hukuwahi kufanya ili tu uwadhihirishie watu kwamba na wewe unaenda na wakati au ni town girl/boy, kumbuka you have no one to prove wrong, you only have you to make proud. Sema HAPANA to anything that doesn’t fit in your standards.

Maisha ya chuo ambayo huna mtu wa kukwambia hiki siyo sawa ni maisha yanayotaka ujijali kwanza mwenyewe laa sivyo kuna wiki utakua unatoka kiwanja kimoja mpaka kingine na hupati hata muda wa kupumzika hakikisha unapata muda wa kupumzika wa kutosha, kula chakula kizuri, na fanya mazoezi.

Kuwa mwaka wa kwanza kusikufanye uingie chuo kinyonge, pambana pigania ndoto zako chagua nani awe rafiki na nani abaki kwenye zone ya watu unao wajua basi  keep motivating yourself every single day kila kitu kinawezekana. ouyaaah weeeh karibu sana chuoni chuo ni bata bwana enjoooooy!!!!!!!
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags