Mwaisa: waliamini nimepotea kuingia kwenye vichekesho, lakini Mungu ameblesi

Mwaisa: waliamini nimepotea kuingia kwenye vichekesho, lakini Mungu ameblesi

Wakati baadhi ya vijana wakisubiri kuajiriwa mchekeshaji Hakika Nyonyoma Mwapongo maarufu kama Mwaisa Mtumbad anasema anaamini kwenye kujiajiri na siyo kuajiriwa.

Anasema imani hiyo ya kujiajiri ndiyo ilipelekea aache kazi Serikalini aliyokuwa akifanya kama Afisa Misitu na kuamua kuingia kwenye tasnia ya uchekeshaji.

Mwaisa ameeleza kuwa hakuna mwalimu mzuri kama njaa kwani ndiyo ilimsababisha aachane na kuajiriwa licha ya kupata kazi hiyo mwaka 2017.

“Hakuna mwalimu mzuri kama njaa kwanza mimi nilikuwa mwajiriwa serikalini ikatokea kuna baadhi ya wafanyakazi tukasimamishwa kazi kwa hiyo wenzangu walienda kufanya shughuli nyingine kama kilimo lakini nikafikiria kama naweza kuwachekesha zaidi ya watu watatu tukiwa tunapiga stori kwa nini nisitengeneze kitu kama vichekesho ndiyo nikanza.” Anasema Mwaisa.

Haikuishia hapo ameeleza kuwa kwa wakati huo alikuwa anafikiria kutengeneza maokoto mengi kwa hiyo aliona kufanya biashara au kilimo ni kama kupoteza pesa


“Mimi nilikuwa nafikiria pesa zaidi kuliko kitu chochote kwa wakati huo so niliposimamishwa kazi mimi sikuwahi kufikiria kuwekeza pesa kwenye kilimo au biashara niliona kama nafukia kibunda tu nikaingia kwenye sanaa ya vichekesho” Anasimulia.
Mchango wa mkewe kwenye sanaa yake
Mwaisa ameiambia Mwananchi Scoop kuwa support kubwa ya kuingia katika sanaa ya vichekesho ilitoka kwa mke wake.
“Wakati naanza sanaa nilikuwa naona vituko sana lakini mke wangu alikuwa ananiunga mkono kuna muda alikuwa anachukua clip ambazo nilikuwa nafanya anaenda ku-share na marafiki zake kazini so walivyokuwa wanaona walikuwa wanapenda sana” Anasema Mwaisa.

Kuajiriwa ni kupoteza muda
“Muda wa masaa tisa ambayo unayapoteza kufanya kazi za watu ndiyo masaa mambayo unaweza kutengeza kitu chako kikawa kikubwa na kikakuletea faida kuliko ungetumia kuajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi za watu” Anasema .

Hata hivyo amedai katika kuajiriwa kunamfanya mtu kutokuwa na uhuru wa kufanya mambo mengine kwa wakati sahihi
“Kitu kingine ambacho kina cost katika kuajiriwa ni kutokuwa na uhuru wa kufanya mambo yako mengine maana kila siku utakuwa unafanya kazi za watu kwa ajili ya kulinda kibunda (fedha)” Anasimulia.


Waliamini nimepotea kungia kwenye vichekesho
Katika kujitafuta sio kila mtu atakuamini kwa asilimia kubwa kwa upande wa Mwaisa anasimulia kuwa wakati ameanza sanaa kuna baadhi ya wafanyakazi wenzake aliyowahi kufanya nao kazi walikuwa wanaona kama amepotea kuingia kwenye comedy.

“Unajua kuna baadhi ya wafanyakazi wenzangu serikalini waliamini nimepotea kufanya vichekesho lakini hilo mimi halikunipa shida kwa sababu nilikuwa nafanya kile ninachoamini, basi Mungu aka-bless mpaka hii leo nazingatia maokoto” Anasema.

Sanaa imempatia vipi faida?
“Comedy imenipatia faida nyingi sana nainaendelea kunipatia faida nyingi tu kama kuwa balozi katika kampuni mbalimbali, na kupata mashabiki wengi, leo hii najulikana hata na mtoto mdogo kupita jina la Mwaisa na kazi zake” Anasimulia.
Pia anasema anapata urahisi wa kuongea na viongozi wakubwa kama mawaziri na kufahamina nao.

“Kupitia sanaa imenisaidia kupata urahisi zaidi kuonana na viongozi wakubwa, ku-share nao stori mbalimbali tofauti na hapo mwanzo kabla sijaingia kwenye vichekesho kwa sabababu hakuna mtu ambaye alikuwa ana nifahamu kwa ukubwa huo kama hivi sasa” Anasema.

Pesa kwanza umaarufu baadaye
“Kwanza mimi nilikuwa sipendi kufahamika sana lakini sina budi kwa sasa nikubali mimi ni maarufu japo nilikuwa sipendi kabisa nilichokuwa nafikiria kwangu ni kusaka bunda (fedha) tu kwa sababu kipindi hicho nilisimamishwa kazi” Anasema Mwaisa.

Mwaisa ameelza kuwa umaarufu ulimfuata na hana budi kukubiliana nao na hakuwahi kuwaza kuwa kupitia sanaa atakuwa kwenye mabango kupitia matangazo mbalimbali ambayo yanafanya azidi kukuwa na kutamani kufanya zaidi ya hapo.
“Huwezi kuzuia Mungu ame-bless vitu ambavyo sikuwahi kuwaza kama vitakuwa hivyo kuhusu umaarufu ambao sikuutaka bali ulikuja wenyewe na sina budi kukabiliana nao kwa sababu kama sasa hivi hadi kwenye mabango kila sehemu nipo hali ambayo inazidi kuniongezea umaarufu” Anasema Mtu Mbad.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags