Muuza vitafunwa mwenye muonekano wa kipekee

Muuza vitafunwa mwenye muonekano wa kipekee

Wanasema jinsi utavyopenda na kuitunza kazi yako ndivyo watu wengine wataiheshimu. Mfahamu Jideobi Chiamaka Favour mwanadada kutoka nchini Nigeria ambaye amewashangaza wengi kupitia mitandao ya kijamii kutokana na muonekano wake wa tofauti akiwa anauza vitafunwa.

Baada ya kumaliza elimu ya Sekondari Chiamaka aliamua kurudi kijijini kwa wazazi wake ambapo alianza kumsaidia mama yake kufanya biashara ya bagia (Akara) siku zote akiwa na wazazi wake alikuwa na ndoto ya kusoma elimu ya chuo kikuu changamoto pekee ikiwa ni uwezo wa wazazi wake kumsomesha.

Aliamua kuondoka kijijini, kwenda mjini kwa lengo la kutafuta kazi, baada ya mishahara wake kutokidhi mahitaji yake ndipo alipata wazo la kufanya biashara anayofanya mama yake kijijini.

Novemba 2018 alianza biashara ya bagia, akiziuza barabarani, kutokana na biashara kutokuwa nzuri akaamua kutafuta sehemu na kuboresha biashara yake kuanzia muonekano wa mavazi na vitafunwa vyenyewe.

Mwaka 2019 alipata nafasi ya kujiunga na chuo Kikuu cha Nnamdi Azikiwe, aliweza kujilipia ada mwenyewe kutokana na pesa alizokuwa akizihifadhi, ambapo alijisomesha kwa miaka 4, mwezi Desemba mwaka jana alihitimu masomo yake.

Kupitia mahojiano yake na ‘Iya Magazine’ aliweka wazi kuwa haikuwa rahisi kwake kufanya biashara huku unahudhulia masomo lakini kwa upande wake alijiwekea ratiba ambayo alikuwa akiifuata kila siku.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags